January 27, 2021



MWAMUZI wa mchezo wa Paolo Valeri alimuonyesha kadi nyekundu nyota wa Klabu ya AC Milan, Zlatan Ibrahimovic kwenye Milan Dabi na kumfanya ashindwe kutimiza jukumu lake la kuipa ushindi timu yake.

Tukio hilo lilitokea Uwanja wa San Siro kwenye mchezo  ambao ulikuwa ni hatua ya robo fainali ya Coppa Italia.

Kwenye mchezo huo wa Coppa Italia uliochezwa Januari 26, Ibrahimovic alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 58 kwa kuwa alionyeshwa kadi mbili za njano.

Kwenye mchezo huo pia nyota huyo mbabe aliingia kwenye vita ya maneno na nyota wa zamani waliyecheza naye ndani ya Manchester United, Romelu Lukaku ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya Inter Milan.

Dakika 90 zilikamilika kwa Inter Milan kushinda mabao mawili ambayo yalifungwa na Lukaku dakika ya 71 kwa penalti na lile la ushindi lilifungwa na Christian Eriksen dakika ya 90+7.

Ericksen alipachika bao hilo akitokea benchi kwa pigo huru hivyo wanatinga hatua ya nusu fainali wakisubiri kucheza na Juventus ama SPAL ambao wanacheza leo mchezo wao wa robo fainali.

AC Milan bao lao lilipachikwa na Zlatan mwenyewe dakika ya 31 ambaye hakumaliza dakika 90 na kushuhudia timu yake ikiambulia kichapo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic