January 27, 2021


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa nyota wao wawili bado wapo kwenye uangalizi wa jopo la madaktari kabla ya kurejea uwanjani.

Kwa sasa kikosi hicho ambacho kinanolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze kimeshawasili kambini na kilianza mazoezi rasmi Januari 25,Kigamboni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa maendeleo ya wachezaji wao wawili ambao ni Saido Ntibanzokiza na Yacouba Songne ni mazuri.

"Wachezaji wetu wote ambao wameshawasili kambini wanaendelea vizuri na tayari mazoezi yanaendelea ambapo ni Saido na Yacouba hawa bado hawajawa kwenye ubora wao.

"Wapo kwenye uangalizi wa jopo la madaktari na tunaamini kwamba watakuwa imara na watarejea uwanjani,".

Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 18.

Saido yeye alipata majeraha kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela na Yacouba alipata majeraha kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Azam FC.

Ilikuwa ni kwenye Kombe la Mapinduzi uliochezwa Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic