KLABU ya Al Hilal leo Januari 26 imewasili ardhi ya Tanzania ikitokea nchini Sudan kwa ajili ya maandalizi ya Simba Super Cup.
Mashindano ya Simba Super Cup yanatarajiwa kuanza kesho Januari 27 ambapo Al Hilal watafungua kwa kucheza mchezo dhidi ya wenyeji wao Simba.
Kwenye mashindano haya ambayo yamezinduliwa na Klabu ya Simba, kuna timu tatu ambazo zinashiriki mashindano haya ambapo yatafanyika Uwanja wa Mkapa majira ya saa 11:00.
Al Hilal ya Sudan na TP Mazembe ya Congo hawa ni washiriki wageni huku Simba wakiwa wenyeji na wote wanashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mbali na maandalizi kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika pia ni kwa ajili ya kukuza uchumi wa timu hiyo ya Simba.
Kiingilio ni buku mbili mzunguko, VIP B & C ni buku kumi na tano huku VIP A ikiwa ni buku 25.
0 COMMENTS:
Post a Comment