January 26, 2021

 


 

ALIYEKUWA kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo  amesema kuwa anavutiwa na viwango vya ubora wa nyota wa Simba huku akitabiri kuwa klabu hiyo msimu huu itafika mbali kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika.

Zahera ametoa kauli hiyo wakati ambapo Simba inajiandaa na michuano ya Simba Super Cup itakayoanza kutimua vumbi kesho na kushirikisha timu tatu ambazo ni; TP Mazembe ya DR Congo, Al Hilal ya Sudan na wenyeji Simba.

Michuano hiyo ni muhimu kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya hatua ya makundi ya  Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Simba imepangwa kundi A ikiwa na timu za Al Alhly ya Misri, As Vita ya DR Congo na Al Merrikh ya Sudani.

Akizungumzia ubora wa wachezaji wa Simba Zahera amesema: "Naamini Simba msimu huu itafika mbali katika ligi ya mabingwa kwa sababu wachezaji wengi wana uwezo wa michuano yenyewe.

"Lakini pia wamepata bahati ya kukutana na timu ambazo walishacheza nazo katika hatua hiyo misimu miwili iliyopita hivyo, ni suala la wao wenyewe kujipanga vizuri.

“Angalia mtu kama  Chama, Kagere au Bocco (John), wote wamesheza msimu mmoja uliopita na walifanya vizuri sasa unadhani safari hii nini kitatokea na ikizingatiwa wamesajili wachezaji.

"Halafu kuna michuano ya Simba Super Cup ambayo ni wazi itawasaidia sana, naamini wanaweza kushangaza Afrika,” 

16 COMMENTS:

  1. Ikiwa usajili wa Simba umekukosha, bila ya shaka Simba dtar hao hawakuwapata kwa bei chee, hivyo basi ni vipi hivi juzi tu ulitamka kuwa Simba hawana uwezo wa pesa za kumleta yule kocha wa Vita Sports Club?

    ReplyDelete
  2. Unatafuta nafas yakuajiliwa simba nahiv umesikia wakikutaja

    ReplyDelete
  3. Zahera kama chizi make, unaanza kuzungumzia timu nyingine kabra kuiweka bora timu yako ujinga mtupu

    ReplyDelete
  4. Zahera,Coach mzuri ni Yule anaye andaa timu kuwnzia chini.Unasifia Kazi za wenzako?! Umefeli kabla hujafanya mtihani ?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kauliza opinion yake kwa kikosi cha Simba na yeye ameongea kitaalamu hana kosa... Mwandishi wa habari ndio kaipindisha habari kwa sababu mtu hawezi tu kuanza kuongea bila kuulizwa kitu jiongezeni na nyie mbumbumbu!

      Delete
    2. Ni hakika zahera hana kiwango cha kukochi timu yoyote Tanzania

      Delete
  5. Mtaalamu anayejielewa hawezi ku comment kuhusu timu ambayo sio yake kama sio mwandishi wa habari au mchambuzi.
    Hata kama akiulizwa.

    ReplyDelete
  6. Nakukubari sana Simba nguvu moja atubagui

    ReplyDelete
  7. Kwani unanafasi gani kwenye kikosi hicho??????

    ReplyDelete
    Replies
    1. Msaidizi wetu huyo anastahili kutoa maneno ya kuipatia timu uhakika wa kukufanya vizr

      Delete
  8. Njaa haipendezi mtu anajinogesha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic