KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Simba, Luis Miquissone 'Konde Boy' amewasili rasmi leo jijini Dar es Salaam akitokea nchini Msumbiji, alipokuwa kwa ajili ya mapumziko mafupi na anatarajiwa kujiunga na kambi ya Simba inayojiandaa na mashindano ya Simba Super Cup.
Miquissone alikuwa sehemu ya
nyota wa Simba waliopewa ruhusa ya kwenda kupumzika baada ya timu hiyo kufanikiwa
kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Afrika ambapo Simba iliiondosha FC
Platimun kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-1.
Miquissone aliyehusika kwenye
mabao nane ya Simba akifunga bao moja na kuasisti mara saba kwenye michuano ya
Ligi Kuu Bara, alikosekana katika michuano ya kombe la Mapinduzi iliyomalizika
kwa Yanga kuibuka na ubingwa baada ya kuifunga Simba kwa changamoto ya mikwaju
ya Penalti 4-3.
Michuano ya Simba Super Cup
itakayoshirikisha timu tatu za Simba, TP Mazembe na Al Hilal inatarajiwa kuanza
kutimua vumbi kesho kwenye uwanja wa mkapa ambapo Simba wataianza karata yake
kwa kucheza dhidi ya Al Hilal ya Sudan.
0 COMMENTS:
Post a Comment