January 19, 2021

 



BAADA ya kurejea uwanjani na kufanikiwa kuhusika katika mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 2-0 iliyoupata Azam dhidi ya Mlandege mshambuliaji wa Azam, Prince Dube ametamba kuwa ataendelea kufunga kama ambavyo aliuanza msimu huu.

Dube alikuwa nje ya Uwanja tangu Novemba 25, mwaka jana baada ya kuvunjika mkono wake wa kushoto kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga uliopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, Jijini Dar es Salaam. 

Kabla ya kupata majeraha hayo Dube alikuwa tayari amehusika kwenye mabao 10 ya Azam kwenye Ligi Kuu Bara akifunga mabao sita na kuasisti mara nne kiasi cha kumkalisha Kagere ambaye alikuwa na mabao manne pekee wakati huo. 

Akizungumzia matarajio yake baada ya kurejea uwanjani Dube amesema: “Kwanza niseme namshukuru Mungu kwa kurejea tena uwanjani baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha ya kuvunjika mkono niliyoyapata mwezi Novemba mwaka jana.

"Lakini pia nawashukuru wale wote ambao walikuwa sehemu ya matibabu yangu na kufanikisha mimi kurejea tena uwanjani. 

“Niliahidi kwamba nitarejea uwanjani nikiwa bora zaidi na nafurahi kuona nimefanikiwa kuhusika kwenye mabao mawili tuliyoyapata dhidi ya Mlandege licha ya kwamba tulipoteza mchezo uliofuata dhidi ya KMKM.

“Naamini nitarejea tena kwenye kasi yangu ya ufungaji kama ambavyo ilikuwa mwanzoni mwa msimu huu, hivyo Kama nilivyoahidi ya kwamba nitarejea uwanjani nikiwa bora zaidi ndicho ambacho nitakifanya,” .

Kwa msimu wa 2020/21 Dube ameweza kumzuia mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere kwa upande wa tuzo ya mchezaji bora akiwa nayo moja kabatini huku Kagere akiwa hajaweza kupata tuzo.


 


5 COMMENTS:

  1. Muwe mnaandika basi alihusika vp alitoa pasi za mwisho au ilikuwa wafungaji kinanani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hawajui waandike nini ili habari iwe bora wanachojali ni heading tu ya kumvuta msomaji... Sijui watajirekebisha lini hawa jamaa

      Delete
  2. Sijaelewa, alimtuliza vipi kagere? Au ni copy and paste ya heading? Kuweni makini jamani

    ReplyDelete
  3. Hongera kwa kupona na kurejea uwanjani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic