January 19, 2021




KOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Etienne Ndayiragiuje amethibitisha kuwa ataikosa huduma ya mshambuliaji wake John Bocco kutokana na mchezaji huyo kuwa majeruhi. 

Majira ya saa 1:00 usiku kwa leo kwa saa za Afrika Mashariki katika mji wa Limbe nchini Cameroon, kikosi cha Stars kitaanza rasmi kampemi yake kwenye michuano hiyo ya CHAN pale watakapocheza mchezo wao wa kwanza wa kundi D dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia.

Akizungumza kuhusu maandalizi ya Stars kwenye mchezo huo Ndayiragije alisema: "Maandalizi ya kikosi chetu yapo vizuri, naamini vijana wangu watawashangaza watu wengi kwenye mashindano haya, nawajua vizuri Zambia.

"Natarajia kukosa huduma ya mshambuliaji wangu John Bocco ambaye alipata majeraha, lakini nina Wachezaji wengine katika nafasi ya ushambuliaji ambao wapo tayari kupambana na kutetea Taifa lao"

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic