January 15, 2021



UONGOZI wa Simba umesema kuwa jina la aliyekuwa kocha wa timu hiyo Patrick Aussems limekuwa likitajwa kuwa miongoni mwa warithi wa mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye amebwaga manyanga ndani ya kikosi hicho.

Sven ambaye alipokea mikoba ya Aussems, msimu wa 2019/20 alisepa ndani ya Simba Januari 7 ikiwa ni siku moja baada ya kukipeleka kikosi hicho hatua ya Ligi ya Mabingwa Januari 6 kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum. 

Kwenye mchezo wa kwanza, Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe na waliweza kupindua meza, Uwanja wa Mkapa.

Kwa sasa Simba ambao ni washindi wa pili wa Kombe la Mapinduzi ambalo limekwenda kwa majirani zao, Yanga baada ya kuwashinda kwa penalti 4-3 ipo mikononi mwa Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola ambaye ni mzawa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Anorld Kashembe, Katibu Mkuu wa Simba amesema kuwa walimu wengi wamekuwa wakitajwa kupokea mikoba ya Sven hivyo mchakato huo unaendelea

"Wanatajwa wengi kuja ndani ya Simba hata huyo unayesema Aussems, (Patrick), hizo ni tetesi, mambo yakikamilika lila kitu kitakuwa sawa.

"Mchakato bado unaendelea na ni kweli kuna majina mengi  ya wanaohitaji kuifundisha Simba, ipo wazi Simba ni taasisi kubwa hivyo kila mmoja anapenda kufanya kazi ndani ya timu hii, mashabiki wasiwe na mashaka," .

Aussems alisitishiwa mkataba wake ndani ya Simba kwa kile walichoeleza kuwa ni mwendo mbovu wa timu hiyo baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali na UD Songo.

Wote wawili wanatokea nchini Ubelgiji ambapo kwa sasa Sven amepata dili jipya ndani ya timu ya Morocco na Aussems yupo huru akiwa hana timu.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic