January 29, 2021

 


ANAANDIKA Zakaria Thabit, Ofisa Habari wa Azam FC 


Januari 30, 2021, Azam FC itacheza mechi ya kirafiki na KMC kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.


Mechi hii itakayoanza saa 10:30 jioni, ni muendelezo wa maandalizi ya Azam FC kuendelea raundi ya pili ya Ligi Kuu.


Mwalimu George Lwandamina anataka kuendelea kujua maendeleo ya kiufundi ya timu yake baada ya mazoezi yaliyoanza Jumatatu, Januari 25 baada ya kurudi kutoka Zanzibar. 


Prince Dube aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu, amepona na anaendelea kujiimarisha kiutimamu wa mwili na kisaikolojia kwa sababu akili yake bado ilikuwa inaogopa sana kujitonesha.


Kipa Mathias Kigonya aliyesajiliwa dirisha dogo, naye anaendelea kuzoea mazingira na mechi hizi za kirafiki ni muhimu kwake katika kuijua zaidi timu yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic