January 29, 2021



ETTIENNE Ndayiragije, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa haikuwa bahati ya timu hiyo kuweza kutinga hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Chan nchini Cameroon. 

Benchi la ufundi la Stars lipo mikononi mwa Ndayiragije ambaye anafanya kazi kwa kushirikiana na Seleman Matola pamoja na Juma Mgunda ambao ni wasaidizi wake.

Ikiwa Cameroon wakati ikishiriki michuano ya Chan ambayo inawahusisha wachezaji wa ndani imefungashiwa virago hatua ya makundi baada ya kukusanya pointi nne kwa kuwa ilishinda mchezo mmoja kwa bao 1-0 dhidi ya Namibia na ilifungwa mabao 2-0 dhidi ya Zambia na ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Guinea.

Mechi ya ufunguzi ilipoteza dira ya Stars kwa kuwa wachezaji walipoteza hali ya kujiamini na alianzisha pia kikosi chenye wachezaji wengi ambao hawana uzoefu na mechi za ushindani.

Miongoni mwa wachezaji ambao walianza kikosi cha kwanza na hajawahi kuwatumia kwenye mechi ngumu ni pamoja na mshambuliaji Yusuph Mhilu, Kalos Protus na Edward Manyama.

Ndayiragije amesema:"Haikuwa bahati yetu kusonga mbele licha ya wachezaji kupambana kusaka ushindi. Pia mwamuzi wa mchezo wetu dhidi ya Guinea alifanya makosa mengi ambayo yametufanya tutolewe,".

Kwenye kundi D ambazo zimesonga mbele ni Guinea na Zambia ambazo zote zimekusanya pointi tano kibindoni.


4 COMMENTS:

  1. Hakuna cha bahati... walinzi wanatembea, hawajipangi..wamerundikana sehemu moja. Kuchelewa kumwingiza Mhilu..hata upewe miaka hapo umegota mwisho

    ReplyDelete
  2. Kocha akubali tu kwamba:
    1. Tulizidiwa uwezo,
    2. Tulizidiwa mbinu,
    Timu inapoongoza umilki wa mpira na magoli, ikavipoteza vyote na hatimaye kurudishiwa goli siyo suala la bahati bali ufindi na uwezo.
    Kocha alishindwa kuwasoma Guinea na kuweka mkakati wa kulinda ushindi.
    Mechi ya Zambia na Namibia tulicheza ovyo kabisa kwamba hawezi kusema tulikuwa tunacheza mfumo au style gani.
    Chaguo lake la timu limekuwa halizijibu mbinu za wapinzani. Huwezi kutumia mipira mirefu kwa mabeki warefu wa Guinea!
    Tumepata la kujifunza

    ReplyDelete
  3. Hakuna bahati mbaya hapo, yaani timu imecheza hovyo na mechi ya mwisho hata kujaribu tu kulinda goli hamna unategemea nini. Yote tisa, kumi hatukuwa na maandalizi ya kutosha kama wenzetu, tumeunga unga tuu, harafu kwa muda huo tunawaacha baadhi ya wachezaji wa Simba wenye uzoefu (Mimi ni Yanga) anatupelekea wachezaji wasio na uzoefu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic