MABINGWA wa kihitoria wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC wakiwa wameweka kambi visiwani Zanzibar wameonja joto ya jiwe jana kwa kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya kikosi cha KMKM.
Azam FC ni vinara wa kutwaa mara nyingi taji la Kombe la Mapinduzi ambapo wameweza kufanya hivyo mara tano wakifuatiwa na Simba ambao wametwaa taji hilo mara tatu.
Mwaka 2021 walitolewa na mabingwa wa taji hilo Yanga baada ya dakika 90 kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 kisha kwenye mikwaju ya penalti wakafungwa penalti 4-3.
Jana, Januari 16, Uwanja wa Mao kipa namba moja wa timu hiyo David Kissu hakuwa na chaguo baada ya kuokota nyavuni mwake mabao mawili huku safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Prince Dube ikishindwa kuliona lango la wapinzani wao KMKM.
Mchezo huo ni maalumu kwa ajili ya kujiweka sawa kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na mechi za Kombe la Shirikisho.
Ndani ya Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya tatu ina pointi 32 baada ya kucheza mechi 17 na imeruhusu mabao 11.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa malengo makubwa ya mechi hizo ni kuweza kujiweka sawa kabla ya ligi kuanza.
"Tupo huku kwa ajili ya kuendelea kufanya maandalizi hasa ukizingatia kwamba kuna wachezaji wapya ambao wamekuja na pia wapo wale ambao walikuwa kwenye kikosi kwa muda mrefu ni wakati wa kocha kutengeneza kikosi cha ushindi," .
Kwenye pasha misuli ya kwanza uwanjani hapo dhidi ya Malindi FC, Azam FC ilishinda mabao 2-0 ambapo wafungaji walikuwa ni Mudhathir Yahaya na Idd Seleman,'Naldo'.
0 COMMENTS:
Post a Comment