January 17, 2021


JONATHAN Nahimana, kipa wa Klabu ya Namungo FC ambapo yupo huko kwa mkopo amesema kuwa hesabu zake kubwa ni kucheza soka la kulipwa nje ya nchi kwa kuwa nafasi hiyo inawezekana kwa sasa kutokana na timu hiyo kushiriki michuano ya kimataifa.

Namungo ipo kwenye Kombe la Shirikisho ikiwa imetinga hatua ya mtoano ambapo ikifanikiwa kupenya mchezo wake dhidi ya Waangola itatinga hatua ya makundi.

Kipa huyo raia wa Burundi alikuwa anatajwa kuibukia ndani ya Simba kwenye usajili wa dirisha dogo ila mambo yalibuma baada ya Beno Kakolanya kuonyesha kiwango kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambapo aliifikisha timu hiyo hatua ya fainali.

Nyota huyo amesema:"Kupitia mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho nina amini kwamba itafungua njia ya mimi kucheza nje ya Bongo na kufanya niwe wa kimataifa.

"Nina amini kwamba kila kitu kinawezekana na hilo lipo wazi kwa kuwa tunafuatiliwa na wengi na hilo litafungua njia ya mimi kuwa kipa wa kimataifa,' .

4 COMMENTS:

  1. Swala la Kakolanya mlikuwa mnalitengeneza ili kuuza magazeti

    ReplyDelete
  2. Unamtafutia ulaji Simba! Simba nafac zimejaa aende huko kwa wamchangani atapata nafac
    *Simba sc no vacany*

    ReplyDelete
  3. Hatutaki kipa huyo anatoka pamoja na akina Saido na Kaze waliotufanya tutoke vibaya Zanzibar.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ��������������������

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic