IMERIPOTIWA kuwa nyota wa kikosi cha Liverpool, Georginio Wijnaldum amegomea kuongeza mkataba mpya ndani ya kikosi hicho ambacho leo kinasaka ushindi Uwanja wa Anfield kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United.
Kiungo huyo mkataba wake ndani ya Anfield unameguka msimu huu ambapo amekuwa hataki kuogeza mkataba mwingine kwa kuwa anataka kupata changamoto mpya nje ya kikosi hicho kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2019/20.
Wijnaldum anatajwa kuhitaji kwenda kutumika ndani ya Klabu ya Barcelona inayonolewa na Kocha Mkuu, Ronald Koeman akiamini kwamba itakuwa fursa kwake kucheza zaidi kikosi cha kwanza ndani ya Nou Camp.
Habari zimeeleza kuwa sababu za kugomea kuongeza mkataba ndani ya Liverpool ni kutaka kwenda Barcelona bure kupata changamoto mpya kwa kuwa Barcelona wanatajwa kuwa wanahitaji huduma ya kiungo huyo.
Kwa mujibu wa Daily Mirror, Liverpool ilijaribu kumshawishi kiungo huyo abaki ndani ya kikosi hicho kwa kuwa alikuwa na mchango mkubwa wakati wakipata Kombe la Ligi Kuu England pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya ila jitihada zao ziligonga mwamba.
Sababu ya kiungo huyo kuhitaji kuondoka pia inatajwa ni uwepo wa ushindani wa namba ndani ya Liverpool ambapo msimu huu ilimuongeza kiungo Thiago Alcantara ambaye anacheza nafasi moja na kiungo huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment