INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Yanga, beki wa kati kijana Dickson Job amesema kuwa anaamini atafanya makubwa ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze.
Job ameibukia ndani ya Yanga akitokea Klabu ya Mtibwa Sugar na amesaini dili la miaka miwili kuwatumikia Wanajangwani ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara.
Yanga inaongoza ligi baada ya kucheza jumla ya mechi 18 na kibindoni imekusanya jumla ya pointi 44 na haijapoteza mchezo mpaka sasa.
Maisha yake ndani ya Mtibwa Sugar msimu wa 2020/21 yalikuwa yenye furaha na alikuwa na uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza. Katika mechi 18 ndani ya Mtibwa Sugar alicheza 17 na zote aliyeyusha dakika 90 huku akikosekana kwenye mchezo mmoja mbele ya Mbeya City.
Tayari ameanza maisha mapya ndani ya Yanga huku akiwa na furaha pia kwa kuwa anatimiza ndoto yake ya muda mrefu kwani alikuwa anafikiria kucheza ndani ya timu hiyo jambo ambalo limetimia.
Job amesema:-"Ninafurahi kuwa Yanga nina amini kuwa nitafanya mambo makubwa, ilikuwa ni ndoto yangu kucheza ndani ya Yanga na sasa imetimia.
"Kikubwa ni kufuata maelekezo ya benchi la ufundi, ushirikiano na wachezaji wenzangu pamoja na kufanya kazi bila kusahau ibada hapo nina amini kwamba kila kitu kitakwenda sawa," .
Anafanya jumla ya mabeki wa kati ndani ya Yanga kwa sasa kuwa watano ambapo ni pamoja na Lamine Moro huyu ni raia wa Ghana, Bakari Mwamnyeto, Said Juma, Abdalah Shaibu pamoja na yeye mwenyewe Job.
Job punguza maneno, piga kazi watu watakuona tuu.
ReplyDeleteSUBIRI AONE, ATAPOTEA KAMA TARIQ SEIF KILAKALA
ReplyDelete