January 29, 2021

 


IMERIPOTIWA kuwa Klabu ya Manchester United inayonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunner Solskjaer ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya mshambuliaji wa Klabu ya Roma na mchezaji wa zamani wa Manchester City, Edin Dzeko.

Dzeko alipelekwa kwa mkopo ndani ya Roma, msimu wa 2015/16 akitokea Manchester City ambapo akiwa ndani ya City msimu wa 2011/16 alicheza jumla ya mechi 130 na kutupia jumla ya mabao 50.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34 awali iliripotiwa kuwa Pep Guardiola anamhitaji kabla ya kupotezea dili hilo jambo linalowapa nafasi United kuipata saini yake ili awe mbadala wa Odion Ighalo ambaye amerudi ndani ya Klabu ya Shangai Shenhua,China.

Ikiwa dili lake la kusepa ndani ya Italia na kuibukia England litabuma anapewa nafasi ya kubaki Italia kushiriki Serie A ila atakwenda Inter Milan ambapo kuna uwezekano wa kufanya mabadilishano na Alexis Sanchez ambaye alikipiga ndani ya Manchester United.

Inaelezwa kuwa hayupo kwenye mahusiano mazuri na Kocha Mkuu wa Roma, Paulo Fonseca jambo ambalo linamfanya afikirie kusepa mazima.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic