January 29, 2021


KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa ndani ya uwanja amewaambia wachezaji wake wapambane kusaka mabao mengi ili kujiweka salama ndani ya dakika 90.

Mfaransa huyo ambaye amebeba mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye alibwaga manyanga Januari 7 kwa kile ambacho alieleza kuwa ni matatizo ya kifamilia tayari ameshaanza kazi.

Sven alisepa ndani ya Simba ikiwa ni muda mfupi baada ya timu hiyo kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kushinda mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum, Uwanja wa Mkapa.

Januari 24, Gomes alitambulishwa na kuanza kukifundisha kikosi hicho huku Sven yeye tayari alianza kazi ya kukinoa kikosi cha FAR Rabat ya Morroco. 

Gomes amesema:-"Nimewaambia wachezaji kuwa ushindi mkubwa utatuongezea hali ya kujiamini ndani ya uwanja, hivyo kitu ambacho tunakihitaji ni kushinda mabao mengi zaidi ndani ya dakika 90.

"Tuna kazi kubwa ya kufanya ikiwa ni pamoja na kuwa na kasi pamoja na uimara wa kujilinda haya yote hayatawezekana ikiwa hakutakuwa na spidi katika kutafuta matokeo.

"Nimewaona wachezaji kila mmoja anakitu chake ambacho anacho hilo kwangu ni furaha hivyo nina amini kwamba kadri muda unavyozidi kwenda kila kitu kitakuwa imara".

Mchezo wa kwanza kukaa kwenye benchi, Gomes ameshuhudia vijana wake wakishinda mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal kwenye mchezo wa Simba Super Cup, Uwanja wa Mkapa, Januari 27.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic