Akimtambulisha mbele ya Waandishi wa Habari, Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema Kocha Mkuu mpya wa Simba, Didier Gomes Da Rosa leo Januari 24, 2021 amejiunga nao akitokea Sudan na amesaini mkataba wa miaka miwili.
"Tunamtambulisha kocha Gomes ametokea Al Merrikh ya Sudan na ni raia wa Ufaransa," amesema Barbara Tayari Simba ishamleta kocha wa makipa juzi na ameanza mazoezi na klabu hiyo jana kuelekea mashindano ya Simba Super Cup yatakayoanza Januari 27-31 na kuzikaribisha timu ya TP Mazembe ya DR Congo na Al Hilal ya Sudan.
Gomes ametokea Al Merrikh ya Sudan inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa kundi moja na Simba.
Gomes ameshukuru kujiunga na Simba yenye malengo na ushawishi mkubwa kwa mashabiki. “Nina furaha sana kuwa hapa na tuna nafasi ya kufanya mengi pamoja mbeleni. Timu niliyoondoka niliamua mwenyewe. Nataka kuwepo Simba kwa muda mrefu.”amesema Gomes
MWINYI ZAHERA MKURUGENZI WA UFUNDI
ReplyDeleteUfundi wa tunguri au?
DeleteCv ya kocha iko vizuri...sasa kazi ibaki uwanjani. Kila la kheri kocha karibu ligi kuu bara. Ligi yenye viwanja vigumu...uchawi...ukamiaji...majungu...hujuma...na utovu wa nidhamu....kila la kheri....jitahidi usibebe kwanza nguo nyingi anza na chache😂
ReplyDeleteKaribu kocha na kweli utakuwa kwa muda mrefu sana. This is bongo football
ReplyDeleteHakika kocha mzuri
ReplyDeletemikia fc hata aje molinyo nyie ni wamatopeni tu , maana shida yenu tunajua ilipo
ReplyDelete