KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2020/21.
Kaze ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda
Sven Vandenbroeck wa Simba ambaye amebwaga manyanga na Francis Baraza wa Biashara United.
Yanga chini ya Kaze kwa mwezi huo ilishinda michezo minne na kutoka sare mmoja ikivuna pointi 13 na kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi.
Yanga ilizifunga Ruvu Shooting FC (2-1), Mwadui FC (0-5), Dodoma Jiji FC (3-1) na Ihefu SC 0-3 huku wakitoka sare na Tanzania Prisons FC 1-1.
Hamzingatii criteria za ligi mnapeana kwakujuana,haiwezekan timu ipo kwenye mashindano ya kimataifa haichezi ligi kuu alafu mnaihusisha kwenye kugombea tuzo,huo ni upumbavu vinginevyo mngehusisha na mechi za ligi ya mabingwa wanayoshiriki NAMUNGO NA SIMBA.kwasababu haiwezekani simba aache kucheza mechi za kimataifa aje kucheza ligi kuu au Namunho aache caf champion aje kucheza ligi kuu ili tupate mchezaji bora na kocha bora wa mwezi,angalieni vigezo mbadala.
ReplyDeleteUjinga kwani simba alicheza mechi ngapi December?
ReplyDeleteLeo nilicheka sana, mitaani huko matopolo wanashsngilia kwa nguvu zao zote kwa kocha wao kuchaguliwa kocha bora
ReplyDeleteTFF wanalinganisha ubora wa kocha kwa mechi za hadhi moja au kulinganisha mechi za ligi kuu, za ASFC na za kimataifa pia? Simba wamecheza idadi ya mechi za ligi kuu sawa na za Yanga kwa hiyo Desemba? Hizi tuzo hazina uhalisia
ReplyDelete