January 26, 2021


MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Fiston Abdoul Razak ameijia juu Kampuni ya uwakala ya Heritage Soccer Agency na kuwaita matapeli kutokana na kampuni hiyo kudai haikushirikishwa katika dili la staa huyo kujiunga na Yanga.

Katikati ya wiki hii ilisambaa barua iliyokuwa imewasilishwa katika Shirikisho la Soka la Kimataifa ‘FIFA’, na Shirikisho la Soka Afrika ‘CAF’ na Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ ikidai mshambuliaji huyo amekiuka mkataba na kusaini Yanga bila ridhaa yao kama wasimamizi wake. 

Akizungumzia madai hayo Fiston amesema: “Hao jamaa ni matapeli, hiyo barua nimeiona, nikawapigia simu, nikawatukana na nimewaambia huo mnaofanya ni utapeli na kama wanawafanyia wachezaji wengine huko mtakuwa hamuwatendei  haki hata kidogo.

“Huwa sipendi ujinga na kitu wanachokifanya siyo sahihi kabisa kwa sababu sijawahi kufanya nao kazi, hawajawahi kunipa dili yoyote hata ya majaribio kwa nini waseme hivyo.

"Na ukiangalia hiyo barua yao imekatwa kwa chini, nafanya kazi na wakala watatu ambao ni raia wa Misri ila siyo wao maana hao wanaodai hivyo mmoja ni Mtanzania na tulishagombana,” 

 

 

 

4 COMMENTS:

  1. Hali ngumu, watu wanajaribu kila fursa. Ila utapeli haufai, unataka kula jasho la mtu mwingine kiulaini? Fanya kazi halali

    ReplyDelete
    Replies
    1. HAKUNA UTAPELI MZEE KAMA NI KWELI NI WAKALA WAKE NI HUYU NGOJENI MATOKEO, KISINDA, MUKOKO, CHAMA HUYU NDIYO WAKALA WAO. HUENDA JAMAA KAPIGIKA SASA ANATAKA KULA SUPU PEKE YAKE WAKATI ANASAHAU KUNA WASHIRIKA WAKE NAMBA MOJA KISHERIA.

      Delete
  2. Kama Ni kweli wafate utaratibu kudai haki yao ila kama Ni uongo watafute Njia nyingine ya kupiga pesa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic