January 20, 2021

 


KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, amesema kuwa kiungo wa timu hiyo, Carlos Sténio Carlinhos anatarajia kurejea kikosini kuungana na wenzake baada ya majeraha yake kuendelea vizuri.

 

Kaze alisema baada ya kiungo huyo kukaa nje kwa wiki kadhaa sasa yupo tayari kuanza mazoezi mepesi, ikiwemo kwenda Gym na kufuata programu ya madaktari kisha baada ya hapo ataanza programu nyingine kwa ajili ya maandalizi ligi kuu.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Kaze alisema majeraha ya Carlinhos yalikuwa yanakwenda sawa na ndiyo maana aliamua kumuondoa kwenye kikosi kilichoshiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi ili apate muda wa kuwa fiti zaidi, jambo ambalo limesaidia na sasa yupo tayari kuipigania timu kwenye raundi hii ya pili.

 

“Tunategemea kuwa Carlinhos ataanza mazoezi wiki hii kwani ripoti ya madaktari ilionyesha kuwa anaweza kuanzia Gym.


Kisha baada ya muda ataungana na wenzake kwenye mazoezi ya pamoja kujiandaa na michezo ya ligi kuu,” alisema Kaze.Nyota huyo raia wa Angola aliumia kwa mara ya Oktoba 19, kwenye mazoezi ya timu yaliyofanyika Kigamboni jambo lililopelekea akose michezo kadhaa.

5 COMMENTS:

  1. mchezaji ni wewe Shukuru kobelo wa morogoro hongera na wenzako wooote kwa ujinga

    ReplyDelete
  2. Sio ujinga ni kweli hamna mchezaji hapo

    ReplyDelete
  3. Mwanzo wa msimu hadi mwisho wa msimu mchezaji ni safari za clinic tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic