ARSENE Wenger kocha wa zamani wa Klabu ya Arsenal amesema kuwa mchezaji wake wa zamani Mesut Ozil alichanganyikiwa kutokana na kutokuwa na nafasi ya kucheza ndani ya kikosi cha Arsenal.
Wenger alikuwa ndani ya kikosi hicho msimu wa 1996-2018 ambapo alipofanya kazi na Ozil alikuwa akimpa nafasi kikosi cha kwanza.
Kwa sasa Ozil yupo nje ya Arsenal na anajiandaa kuanza maisha mapya ndani ya kikosi cha Fenarbahce ili kuanza changamoto mpya ambapo atakutana na Mtanzania, Mbwana Samatta.
Wenger amesema:"Hakuwa na furaha na alikuwa kwenye hali ya kuchanganyikiwa kwa kuwa alikuwa hachezi sasa angefanya nini zaidi ya kutokuwa vizuri?
"Ni moja ya wachezaji wazuri ambao wana uwezo wa kutengeneza nafasi na kufunga, anajua hali halisi ya washambuliaji namna wanavyopaswa kupewa mipira pamoja na kukaa sehemu sahihi," .
0 COMMENTS:
Post a Comment