January 20, 2021


 SELEMAN Matola, kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa vijana walicheza vizuri ila makosa yaliwafanya washindwe kupata matokeo ndani ya uwanja.

Matola amesema kuwa nafasi ya kufanya vizuri ipo kwa kuwa wana mechi mbili mkononi za kucheza kwenye mashindano hayo ambayo yanahusisha wachezaji wa ndani.

Jana, Januari 19 Stars ilifungua pazia ndani ya Chan kwa kufungwa mabao 2-0 ambapo moja ilifungwa kwa mkwaju wa penalti na moja kwa shuti kali la nje ya 18.

Matola amesema kuwa wachezaji kipindi cha kwanza walifanya kazi kubwa ya kusaka ushindi ila mambo yalikua magumu kwao na kipindi cha pili makosa waliyofanya yaliwagharimu.

"Wachezaji walicheza vizuri kipindi cha kwanza ila kipindi cha pili makosa ambayo walifanya yameweza kuleta mabao ya kufungwa.

"Naona kwamba bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zetu ambazo zimebaki kikubwa ni kuendelea kutoa sapoti na kila kitakuwa sawa," amesema.

Mchezo unaofuata kwa Stars nchini Cameroon ni dhidi ya Namibia itakuwa ni Jumamosi, Januari 23.

6 COMMENTS:

  1. Kweli nafai ipo ila je uwezo nao upo?

    ReplyDelete
  2. Kweli nafasi ipo ila je uwezo nao upo?

    ReplyDelete
  3. Hamna kitu hapo,turudi nyumbani

    ReplyDelete
  4. Wacha tujifariji kama kawaida yetu

    ReplyDelete
  5. Nafasi ya kufanya vyema kwenye mashindano haya ya chan kwa Tanzania ni madogo sana na huo ndio ukweli. Wasemaji wamekuwa wengi sana mno juu ya timu ya taifa hasa wale wanaojiita Wachambuzi wa mpira wetu. Wanaweka mbele siasa zaidi kuliko kuelezea uhalisia wa tatizo husika kwa wakati husika.Taifa stars ni timu ya watanzania na kila mtanzania anahaki ya kutoa maoni yake hata kama wasimamizi wa timu hawatapenda. Lakini kwa bahati mbaya Sana Kuna baadhi ya Wachambuzi wachache hasa pale wasafi media wapo kisiasa zaidi. Job job yupo vizuri kwenye msimamo wake wengine ni wasanii zaidi. Niwapongeze cloud Fm hasa shafii shauda na timu yake jinsi walivyotoa tasmini yao ya mchezo wa Taifa stars zidi ya Zambia.Tasmin yangu binafsi ya Taifa stars nikwamba.
    (1) Tatizo kubwa la Kwanza lipo kwa jopo Zima linaloisimamia Taifa stars na Kama tunataka kubadilisha timu iwe ya mafanikio zaidi basi watanzania tuanze na kubadilisha jopo zima la wale wanoisimaia timu hiyo.Au angalau Kama Taifa itaondolewa mapema kwenye mashindano haya basi tutarajie wahusika wakijiuzulu wenyewe. Moja ya crucial position au nafasi nyeti kwa timu ya Taifa ni ya Manager. Namuheshimu Sana Haroub ila ni mpole mno na mtu mwenye haya kwa nafasi ile.Ningependa kuona mtu Kama Ali mayai au hata mazee Ismail Aden Rage kwenye hii nafasi na pengine Haroub akahusishwa zaidi kwenye benchi la ufundi zaidi kuliko utawala.
    (2) Simba na Yanga sio tatizo la Taifa stars. Bila ya Simba na Yanga hata mpira watanzania tusingekuwa na habari nao.
    (3)Ni Mambo ya kushangaza ila yanatokea Tanzaniania tu kwa wachezaji wengi wa best team ndani ya nchi kuachwa na timu ya Taifa. Mchezaji mzawa wa Simba anaekaa bechi ni bora kuliko star wa timu nyingi ndani ya team zetu. Utamuachaje Dilunga, Muzamiru,shabalala,hata kenedi juma kwangu mimi ni bora kuliko baadhi ya vijana ndani ya Taifa stars. Wachezaji Kama Muadathiri yahaya,Abrahani Musa,sure boy,Paul ngalema,khasani kabunda,hata Paul nonga ni bora kuliko nchimbi najua wapo wachezaji wengi tu tayari Wana uzoefu lakini kwetu sisi labda tunaona ni wazee ila hakika
    hawa ndio wachezaji halisi wa kuitwa timu ya Taifa na wenzetu ndivyo wanavyofanikiwa hawakimbilii kwa wachezaji wanaong'aa kwenye msimu mmoja wa ligi.Hata Mohamed Issa Banka angetupa kitu Cha maana zaidi ndani ya stars.
    Kwenye mechi ya Zambia timu haikucheza vibaya ila sina Shaka yeyote Taifa stars ingefanya vyema zaidi Kama kungekuwa na uteuzi bora wa wachezaji wa timu ya Taifa hata kama tulikosa maandalizii ya kutoaha na huo ndio ukweli na mwnye kubisha basi anaendelee kubisha tu.

    ReplyDelete
  6. upuuzi tu, nakuambia hatushindi mechi hata 1

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic