KIUNGO mshambuliaji mpya wa klabu ya Simba, Perfect Tatenda Chikwende amefunguka kuwa atahakikisha anacheza kwa kiwango kikubwa akiwa na jezi ya Simba ili kuisadia kufikia malengo waliyojiwekea msimu huu.
Chikwende alitambulishwa rasmi na kikosi cha Simba usiku wa
majira ya saa 5 na dakika 59 siku ya Ijumaa baada ya kukamilisha dili lake
akitokea kwenye kikosi cha klabu ya FC Platinum ya kwao nchini Zimbabwe.
Chikwende alipata dili hilo baada ya kuonyesha uwezo mkubwa
kwenye michezo miwili ya Ligi ya mabingwa Afrika waliyocheza dhidi ya Simba
amnbayo Simba walishinda kwa mabao 4-1 huku bao pekee la Platinum likiwekwa
kambani na Mzimbabwe huyo.
Chikwende anakamilisha listi ya wachezaji wawili tua mbao
Simba imewasajili katika usajili wa dirisha dogo lililofunguliwa rasmi Desema
16 na kufungwa usiku wa Ijumaa ya Januari 15.
Akizungumzia kuhusu kumwaga kwake wino ndani ya klabu ya
Simba, Chikwende amesema: “Nimejiunga na Simba nikijua wazi kuwa hii ni
miongoni mwa klabu kubwa, na naahidi kujituma kwa uwezo wangu wote ili
kuisaidia kufikia malengo yake,”
Enter your comment...Kaza buti
ReplyDeleteSafi sana jembe letu
ReplyDeletepale simba kupata namba kuna kaz ya ziada anatakiwa afanye
ReplyDelete