IMERIPOTIWA kuwa Klabu ya Manchester City inahitaji kupata saini ya nyota wa Inter Milan, Romelu Lukaku.
Pep Guardiola, Kocha Mkuu wa City kikosi chake kimekuwa kwenye mwendo wa taratibu kikiwa kimeachwa kwa jumla ya pointi nne na vinara wa Ligi Kuu England ambao ni Manchester United.
Bado kina mchezo mmoja mkononi dhidi ya Crystal Palace ambao utachezwa leo Uwanja wa Etihad na mwamuzi anatarajiwa kuwa Lee Mason.
Ila City imekuwa ikipata tabu kwenye safu ya ushambuliaji pamoja na safu ya ulinzi ambayo imeruhusu mabao 13 kwenye mechi 16 jambo ambalo linampasua kichwa Pep ambapo nyota wake ikiwa ni pamoja na Sergio Aguero, Fernandinho na Eric Garcia wanahitaji kuondoka kwenye kikosi hicho msimu huu.
Kwa mujibu wa The Telegraph, Guardiola anahitaji mshambuliaji kwenye kikosi chake hivyo anafikiria kuinasa saini ya Lukaku ambaye aliwahi kuwa ndani ya Manchester United.
Pia majeraha ya mara kwa mara kwa raia wa Argentina, Arguero mwenye miaka 32 mkataba wake unameguka baada ya miezi sita huku akionekana kuwa hana nia ya kubaki ndani ya kikosi hicho vinaongeza nguvu kwa kocha huyo kufikiria kumpata mshambuliaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment