BAADA ya kutwaa taji lake la kwanza akiwa na uzi wa kikosi cha klabu ya Yanga, kiungo mshambuliaji wa kikosi hicho Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ amefunguka kuwa ana furaha kubwa kushinda taji hilo na kwa kiwango kikubwa alichokionyesha uwanjani kama alivyoahidi wakati anatua nchini.
Ntibazonkiza ambaye amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Desemba, amekuwa na kiwango kikubwa akiwa na kikosi cha Yanga ambapo ameichezea timu hiyo michezo mitano na kuhusika kwenye mabao saba akifunga mabao manne na kuasisti mara tatu.
Nyota huyo wa kimataifa wa Burundi alitambulishwa rasmi na Yanga Oktoba 12, mwaka jana akiwa kama mchezaji huru.
Akizungumzia mafanikio yake ndani ya kikosi cha Yanga Ntibazonkiza amesema: “Nafurahi kwa kufanikiwa kushinda taji langu la kwanza nikiwa na kikosi cha klabu ya Yanga, haya ni mafanikio makubwa kama mchezaji kwa kuwa kila mchezaji mkubwa anahitaji kuthibitisha uwezo wake kwa kupata mafanikio hususani kushinda mataji.
“Tangu nimefika hapa nchini nilisema mimi siyo muongeaji sana, bali napenda kuonyesha uwezo wangu uwanjani na watu wanijaji kutokea huko, tumeanza na Mapinduzi na sasa mawazo yetu ni kuelekea kwenye mashindano mengine tutakayoshiriki,”
Watu wamemwandama Onyango mzee, hiki mbona pia kikongwe?
ReplyDeleteUzee dawa
DeleteHata khamisi Tambwe alidanganyika kuwa anafuraha ndani ya Yanga akaondoka na kilio.
DeleteHivi ninyi wapenzi wa Simba kila Zuri la Yanga lazima u comment ,ukikaa kimya unakufa?
ReplyDeleteNi utani tuu mtani, usikasirike, acha maisha yaendelee
ReplyDeleteWaachen waongee sana maana wasipo ongea saiv wataongea saangap,mwaka huu wataijua yanga ni Tim gan
ReplyDeleteHata Yikpe alisifiwa hivyohivyo,baadae akafungashiwa virago.
ReplyDelete