KIUNGO mshambuliaji mpya wa klabu ya Simba, Tatenda Perfect Chikwende amesema anaamini uwepo wa mashindano mengi ambayo Simba inashiriki ni miongoni mwa vitu vitakavyomsaidia kukuza kiwango chake.
Chinkwende amejiunga na Simba akitokea kwenye kikosi cha
klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe baada ya kuonyesha uwezo kwenye michezo miwili
aliyocheza dhidi ya Simba.
Simba iliiondosha FC Platinum kwa jumla ya mabao 4-1 na
kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Afrika huku huku bao pekee la
Platinum likifungwa na Chikwende.
Akizungumzia maisha yake mapya ndani ya Simba Chikwende
amesema: “Nipo tayari kutumika kuisaidia Simba, nafurahi kuwepo hapa na najua
nitapata nafasi kubwa yakukuza kiwango changu maradufu kutokana na ukweli
kwamba Simba inashiriki michuano mingi hivyo ni nafasi kwangu kucheza mara kwa
mara,”
Unakaribishwa Simba kwa mikono miwili na utajiona upo katika nyumba ya amani ya upendo
ReplyDeleteKaribu kwenye team ya washindi..
ReplyDelete