January 20, 2021

 


BAADA ya kiungo Mkongo Karim Kinvuid Kiekie kuhusishwa kumalizana na klabu ya Simba, hatimaye kiungo huyo amefunguka kuwa hajafanya mazungumzo na uongozi wa Simba

Kiekie alicheza katika mchezo wa kirafiki kati ya Tanzania na Congo uliofanyika katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar na kumalizika kwa sare ya bao 1-1,kwa sasa kiungo huyo yupo katika kiosi cha timu hiyo kinachoshiriki michuano ya CHAN inayoendelea kufanyika nchini Cameroon.

Akizungumzia kuhusu dili hilo Kiekie amesema: "Sijafanya mazungumzo na Simba juu wao kuhitaji huduma yangu, yote ambayo unayasikia wewe na mimi ninayasikia hivyohivyo ndio maana nayaacha yabaki kuwa tetesi ila kama itatokea wananihitaji basi kila kitu kitafahamika,”

Kiekie mwenye umri wa miaka 19 kwa sasa anakipiga katika klabu ya DC Motema Pembe ya nchini Kongo ambapo  nchini humo anachukuliwa kama mmoja kati ya wachezaji bora wanaochipukia kwa kasi.

1 COMMENTS:

  1. Wewe ndo ulimuhoji au Kuna chombo Cha habari ulisikia akiongea,tatizo la waandishi wetu wengi mnapenda kutunga stori huyo mchezaji kashamalizana na Simba Kama subirini muone tusiandikie mate wakati wino upo(taarifa za ndani za Simba keshatua huyo)

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic