January 20, 2021

 


KOCHA mkuu wa klabu ya Yanga, Cedric Kaze amenogesha shangwe la ubingwa kwa mastaa wa  kikosi hicho baada ya kuwapa mapumziko kamili bila programu yoyote ya mazoezi ili mastaa hao wapate muda wa kukaa na familia zao kabla ya kurejea tena kambini Januari 25.

Yanga Januari 13, mwaka huu ilimaliza ukame wa muda mrefu wa kutotwaa mataji baada ya kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuwachapa Simba kwa changamoto ya mikwaju ya Penalti 4-3.

Kocha huyo amewapa mastaa wake mapumziko mpaka Januari 25 ili kuwapa muda wa kutosha kwa mastaa hao kupumzika kwa ajili ya kuwa tayari kwa michezo ya mzunguko wa pili. 

Akizungumzia mapumziko hayo Meneja wa kikosi cha Yanga, Hafidh Saleh amesema: "Baada ya kazi kubwa ya kutwaa ubingwa wa michuano ya kombe la Mapinduzi, kocha Kaze amewapa mapumziko ya muda nyota wote wa kikosi chetu ili waende kujumuika na familia zao mpaka tarehe 25 ambapo wanatarajiwa kurejea tena kambini. 

“Kocha ameamua kuwapa wachezaji likizo isiyokuwa na program yoyote ya mazoezi ili kuwapa muda wa kutosha nyota hao kupumzika baada ya kazi kubwa waliyoifanya kwenye ligi na kombe la Mapinduzi,”

Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi zao 44 baada ya kucheza michezo 18, hawajapoteza mchezo wowote mpaka sasa.

9 COMMENTS:

  1. Kumbe ubingwa wa kombe la mapinduzi mlifanya kazi kubwa sana kuupata teh teh teh teh da nchi ngumu sana hii

    ReplyDelete
  2. K2ko cha milenia hicho@1st comment

    ReplyDelete
  3. Tatizo wanjitutumua mno kuoata ushindi, washukuru haya Mapumziko maana kwenye ligi kuu bara walishaonekana kuanza kuchoka... Ngoja mzunguko wa pili uanze baada ya mechi kadhaa uone watakavyotaabika

    ReplyDelete
    Replies
    1. hujui mpira wenzako ndio maana wanashidwa kujituma hapo Limbe na Duala CHAN, kaeni na ujinga wenu tu kama vile hamjui hata messi na Ronaldo huwa wanakaba mpira kazi la sivyo utaishia kuwa kama ajibu, kichuya, na mgosi

      Delete
    2. Naona umetaja vyuma vya kimataifa

      Delete
  4. Mnateseka sana na Yanga et mechi za mwisho walichoka yaan sare na prison?ninyi mliwafunga prison?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kuwasihi tu muache ulimbukeni. Mapinduzi Tsh.15m/= makundi club bingwa 1.2b/= Nani anateseka hapo?

      Delete
  5. Yani Messi na Ronaldo unafananisha na UTOPOLO, umewakosea heshima wakina Messi

    ReplyDelete
  6. Duuh hii nayo kali hadi leo Manyani fc wanaweweseka na ubingwa wa mapinduzi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic