CRYSTAL Palace ina matumaini ya kuthibitisha kupata saini ya mshambuliaji wa Klabu ya Mainz, Jean-Philippe baada ya kutua London kwa ajili ya vipimo siku ya Jumatano.
Imeripotiwa kuwa mkataba wake wa mkopo utakuwa ni wa muda wa miezi 18 ambapo kuna malipo ya ada ya uhamiaji ambayo ni Euro milioni 2.7 na una kipengele cha kumnunua kwa Euro milioni 13.4.
Akiwa ndani ya Klabu ya Mainz ambayo alikuwa hapo kuanzia msimu wa 2018 amecheza jumla ya mechi 67 na kutupia mabao 24.
Crystal Palace inaamini kwamba ujio wa nyota huyo utaongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ambayo imekuwa na ubutu kwenye upande wa umalizaiaji.
Mshambuliaji wao wanayemtegemea Christian Benteke ametupia jumla ya mabao matatu na Jordan Ayew ana bao moja pekee jambo linalowafanya wapambane kupata mshambuliaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment