January 20, 2021

 


KOCHA mkuu wa Ruvu Shooting, Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa anaamini uwekezaji mkubwa uliofanywa na Yanga kwa kusajili wachezaji bora ni miongoni mwa sababu kubwa za mafanikio ya kikosi hicho kilicho chini ya kocha Mrundi, Cedric Kaze.

Yanga imekuwa yamoto msimu huu ambapo mpaka sasa ndiyo mabingwa wa kombe la Mapinduzi na vinara wa Ligi Kuu Bara baada ya kukusanya pointi 44 katika michezo 18 waliyocheza, huku wakiwa na rekodi ya kucheza michezo 22 ya mashindano rasmi bila kupoteza tangu kuanza kwa msimu. 

Mkwasa ambaye ameifundisha Yanga katika vipindi tofauti, ambapo msimu uliopita alihudumu kama kocha msaidizi ndani ya kikosi hicho amekuwa na wakati bora msimu huu akiiongoza Ruvu Shooting kukamatia nafasi ya tano kwenye msimamo na pointi zao 28 walizokusanya baada ya kucheza michezo 17.

Akizungumzia ubora wa Yanga msimu huu Mkwasa alisema: “Msimu huu Yanga imekuwa na  bajeti kubwa zaidi hivyo kumpa urahisi kocha kufanya usajili wa wachezaji bora na hata kuwa na kambi zenye mazingira mazuri zaidi, kwa upande wangu hili ni miongoni mwa sababu kubwa za wao kupata mafanikio makubwa waliyonayo”

 

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic