January 21, 2021


JUMA Mwambusi, ameomba kukaa kando kwa sasa ndani ya kikosi cha Yanga kwenye majukumu ya kuwa kocha msaidizi.

Hatua hiyo imefikia baada ya yeye mwenyewe kuandika barua baada ya kikosi hicho kutwaa taji la Mapinduzi ambapo iliifunga Simba kwa penalti 4-3 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila kufungana, Uwanja wa Amaan, Visiwani Zanzibar.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa kwenye barua yake ya kuomba kujiweka kando ametaja sababu kuwa ni kuwa na matatizo ya kiafya.

Ameongeza kuwa ameshauriwa na wataalamu kukaa sehemu ambayo itamfanya asiwe na msongo wa mawazo pamoja na kupiga kelele.

Kwa sasa timu itakuwa chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze raia wa Burundi ambaye ameachiwa jukumu la kusaka msaidizi wake.

16 COMMENTS:

  1. Kocha mkuu, kocha wa makipa na sasa kocha msaidizi atakuwa Mrundi.

    ReplyDelete
  2. Tumuachie kaze mwenyewe atakua yupi sahihi kwake awe mrundi,, mjamaica au mparestina atakua yeye cha msingi aje assistance coach

    ReplyDelete
  3. kwa takwimu ya kaze kwenye vilabu alivyotoka, Mwambusi amevumilia sana kufikia mpaka sasa

    ReplyDelete
  4. Tukigundua analeta ukabila tunatimua wote hatupendi ishu za ubaguzi sisi

    ReplyDelete
  5. Acheni ujinga na kuleta neno ukabila hapa.Atakavyo amua kocha wa Yanga maamuzi yake yaishimiwe katika misingi ya kazi na watanzania tutubu na mawazo ya kishetani ya kufikiria ukabila.

    ReplyDelete
  6. Kama atakuwa na ukabila wa kuleta warundi pekee hatutakubali

    ReplyDelete
  7. muacheni jamani kaze wetu hata team yote iwe waburundi sawa

    ReplyDelete
  8. Head coach:kaze (burundi)
    Msaidizi(burundi)
    Kocha wa makipa(burundi)
    Foward ntibazonkinza(burundi)
    Foward wa pili: fiston (burundi)

    đŸ˜‚bongo sihami

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mpenda mpira Tanzania na shabiki damu wa Simba

      Delete
  9. Kwanza Mimi naona Mwambusi alichelewa maana naye Hana jipya,nimefurahi Sana kujitoa kwake ,hapo utakuta kapigwa majungu kwamba yeye anampa sifa Kaze kwa kumsaidia.Hapa U Tanzania tuweke kando tuwe wa kweli na Elimu yetu .Hapa Kuna Tathnia mbili ufanisi wake uwa unanitatiza kwa Ujumla ,1.Waandishi wa Habari kwa Ujumla wao 2.Makocha wa Michezo haswa Soka.Mbona wao kutoka nje ya Nchi ni Kama kukata Mti utoke damu?Waandishi wakitoka utasikia DW,BBC,VOA nk zote Kiswahili na labda Mkuu was Kitengo Mswahili kutoka Mombasa Kenya ,Zanzibar .Swali hapa huko huwa hamtoshi?Lkn kwa kukosoa hata Guadiola mnamzidi Kufundisha.Makocha utawasikia Oman au Mombasa.

    ReplyDelete
  10. Kwa hiyo anarudi Mbeya City kuishusha daraja au vipi hana jipya nae bora aende tu sawa kapumzike salama bro Mungu akupe afya njema zaidi Amin

    ReplyDelete
  11. Mungu akutangulie,kila mmoja ufanya kazi kwa mtu anaemuamini,hata viongozi wa kiselikari uchagua watu wao wanaowamini kufanyanao kz hawe ndugu au asiwe ndugu mnatakiwa kujua ilo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic