WILLIAN nyota mpya ndani ya kikosi cha Arsenal kilicho chini ya Kocha Mkuu, Mikel Arteta amesema kuwa ni ngumu kupata namba jumlajumla kikosi cha kwanza kwa kuwa bado hajaweza kwenda sawa na falsafa ya timu hiyo.
Nyota huyo ambaye aliibuka ndani ya Arsenal akitokea Klabu ya Chelsea inayonolewa na Frank Lampard amekuwa akisugua benchi mara kwa mara baada ya kuibuka kwa usajili wa bure kwa kuwa mkataba wake ulikuwa umeisha ndani ya kikosi alichokuwa.
Wengi walimtabiria makubwa ila imekuwa ngumu kufanya hivyo ambapo amecheza jumla ya mechi 18 na kutoa pasi tatu za mabao.
Nyota huyo amesema:"Nimekuwa ndani ya Uwanja wa Stamford Bridge kwa muda wa miaka 7, kwa sasa nimeanza maisha mapya ndani ya Arsenal hivyo kuna falsafa ambayo lazima niifuate.
"Licha ya kuwa kwenye wakati huu niliopo kwa sasa ninajiskia vizuri na ninapenda kile ambacho ninakifanya hivyo bado ninaamini kwamba nitakuwa bora," .
0 COMMENTS:
Post a Comment