KIUNGO wa Klabu ya Manchester United, Paul Pogba amesema kuwa hawapo hatua moja na wapinzani wao Liverpool licha ya wao kuwa vinara wa Ligi Kuu England kwa sasa ila watapambana wawafunge watakapokutana uwanjani.
Manchester United inatarajiwa kukutana na Liverpool ambao ni mabingwa watetezi Jumapili ya Januari 17, Uwanja wa Anfield ambapo mwamuzi wa mchezo huo anatarajiwa kuwa Paul Tierney.
Mabingwa watetezi Liverpool wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi zao 33 wanakutana na vinara Manchester United ambao wana pointi 36 na wote wamecheza jumla ya mechi 17 msimu wa 2020/21.
Kiungo huyo ambaye amekuwa akitajwa kuwa anaweza kuondoka msimu huu amesema kuwa wanakwenda kupambana na Liverpool ya Jurgen Klopp ambayo ni imara ikiwa Uwanja wa Anfield.
Ole Gunnar Solskajaer ameanza kumuamini kiungo wake huyo akiamini kwamba atakuja kuwa bora kwenye mechi zake zijazo ndani ya Manchester United kwenye mechi zake zote za ushindani.
"Tuna kazi ya kufanya na kuonyesha kwamba tumeimarika licha ya kwamba tunaonekana kuwa imara bado hatujafikia malengo yale ambayo tunayahitaji ndani ya uwanja.
"Kiuhalisia kwa sasa hatuwezi kusema kwamba tupo sehemu moja na Klabu ya Liverpool ndani ya Ligi Kuu England, ila wao wameshinda taji la Ligi Kuu England ni lazima tuwaheshimu.
"Ikiwa unahitaji kuwa bora ni lazima umshinde yule ambaye ni bora ndani ya uwanja, kwa sasa tunajua kwamba wao wameshinda taji la Ligi Kuu England, tunahitaji kumpiga bingwa wa Ligi Kuu England," amesema Pogba.
Liverpool itaingia uwanjani bila ya uwepo wa beki wao tegemeo namba moja Virgil van Dijk na Joe Gomez ambao wana majeraha ya muda mrefu.
Gdr =p~
ReplyDelete