January 17, 2021

 


UONGOZI wa timu ya Yanga unatarajia kutoa kitita kisichopungua milioni 300, kwa benchi la ufundi la timu hiyo pamoja na wachezaji kama sehemu ya kuwapongeza baada ya kuibuka na ubingwa wa michuano ya Mapinduzi.

Fainali hiyo ya Mapinduzi iliyofanyika Jumatano iliyopita katika Uwanja wa Amani Visiwani Zanzibar, ilishuhudiwa na mabosi wote wa Yanga wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa GSM ambao ni wadhamini wa Yanga, Ghalib Said Mohamed, Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM Injinia Hersi Said, Mwenyekiti wa Yanga Dk. Mshindo Msolla na Mshauri mkuu wa mabadiliko wa Yanga Senzo Mbatha Mazingisa.

Chanzo cha kuaminika ndani ya Yanga kililiambia kimesema kuwa, kabla ya mchezo kufanyika mabosi walitoa ahadi ya milioni 200 kama wangeweza kutwaa kombe hilo lakini baada ya kufanikiwa kutwaa waliongeza fedha kutoka milioni 200 mpaka 300.

“Baada ya Yanga kutinga hatua ya fainali na wakajua kuwa wanaenda kucheza dhidi ya Simba katika fainali hiyo viongozi wa Yanga walikaa na wachezaji  na kuzungumza ili kujua ni namna gani wataweza kuutwaa ubingwa huo.

“Hivyo kupitia kikao hiko mabosi wa Yanga waliahidi kiasi cha milioni 200 kwa wachezaji wa Yanga ili kuwaongezea hali ya kupambana, kuhakikisha kuwa wanabeba kombe mbele ya watani wao Simba.

“Chaajabu baada ya kufanikiwa kutwaa kombe hilo kwa changamoto za mikwaju ya penati 4-3, viongozi na mabosi wa Yanga wakaongeza kiasi cha fedha kutoka milioni 200 mpaka kufikia milioni 300 na kupelekea furaha kubwa kwa wachezaji na benchi la ufundi ambalo limeahidi kuutwaa na ubingwa wa ligi kuu, ambapo nyota hao wanatarajia kupewa fedha hizo," kilisema chanzo hicho.


6 COMMENTS:

  1. Afadhali wameambulia hizo maana hakuna kombe lingine tena watatwaa labda wajaribu tena msimu ujao

    ReplyDelete
  2. Kamba tupu, wskipeea wakatambike

    ReplyDelete
  3. Kamba tupu. Wakipewa wakatambike

    ReplyDelete
  4. We mbumbu kaongelee used zenu hizo inakuhusu Nini?

    ReplyDelete
  5. Hongereni viongozi wetu wa yanga nawaamini

    ReplyDelete
  6. Mgeukie mwenzako mwambie Yanga inakupenda

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic