January 23, 2021

 


 UNAAMBIWA uongozi wa klabu ya Simba ulitumia umafia mkubwa kumalizana na kumsainisha kiungo mkabaji wao mpya raia wa DR Congo, Daxo Gikanji kwa kutumia mchezo wa kirafiki kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya DR Congo uliofanyika katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar siku ya Januari 12, mwaka huu.

Licha ya kutokucheza lakini, Gikanji alikuwepo katika kikosi timu ya taifa ya Congo kilichokuja nchini Tanzania kucheza mchezo huo wa kirafiki ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 japo.

Akizungumzia namna dili hilo lilivyokamilika Gikanji amesema: “Baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Tanzania na Congo tulimalizana kila kitu na viongozi wa Simba hadi suala la kusaini mkataba, tayari mazungumzo yalikuwa yameshakamilika kabla ya mimi kuja Tanzania kilichobaki kilikuwa ni mimi kusaini tu hivyo tulitumia nafasi ya mchezo ule kukamilisha usajili wangu.

“kwakuwa tulikuwa tukijiandaa na safari ya kwenda nchini Cameroon kwa ajili ya mashindano ya CHAN siku moja baada ya kumalizika kwa mchezo ule ndiyo maana tulionana na kumaliza kila kitu.

“Nafurahi kuwa mchezaji wa Simba, malengo yote ya Wanasimba itabidi yawe malengo yangu pia kwa kuwa kwa sasa mimi ni familia moja nao,”

 

8 COMMENTS:

  1. Tumshukuru Mungu jinsi mambo yanavokwenda kiulaini kabisa shusri kama maji ndani ya mtungi bila ya makeke. Tunastukia neema

    ReplyDelete
  2. Sasa hao wote wanacheza michuano ipi?

    ReplyDelete
  3. Hivi sie mbona wachezaji wetu tunawapokeaga kimyakimya hatujanagi airport kama wale wenzetu,dah kweli Simba timu kubwa.

    ReplyDelete
  4. Wewe inakuhusu nini? Peleka ujinga huko jangwani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic