January 23, 2021

 


 BAADA ya tetesi kuenea kuwa simba imemalizana na kocha mkuu wa DR Congo na AS Vita, Florent Ibenge kuwa kocha wao mkuu, hatimaye kocha huyo ameweka hadharani kuwa hajasaini kuifundisha timu hiyo bali alikutana na Simba kwa ajili ya kuongelea kuhusu maendeleo ya soka.

Ibenge kwa sasa yupo nchini Cameroon akiwa na timu ya Taifa ya Congo ambayo kwa sasa inashiriki michuano ya CHAN.

Akizungumzia lengo la kuonana na Ofisa mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Ibenge amesema: "Ni kweli nilikutana na CEO wa Simba na kufanya nae mazungumzo yalikuwa mengi ya kawaida lakini pia yalihusisha kuhitajika kuifundisha timu hiyo ambapo hayakufanikiwa.

“Lakini ukiachana na maombi hayo ya Simba tuliweza kuongea mambo mengi kuhusu maendeleo ya mpira hasa kwa kuwa sisi ni majirani na tunashirikiana katika vitu vingi,"


3 COMMENTS:

  1. IBENGE NI POSITIVE COVID 19, LINI ALIONGEA NA BARBARA GONZALEZ? LINI ALIKAA NA WAANDISHI WA HABARI?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe upo dunia gani?kila siku picha inasambaa harafu unauliza lini.

      Delete
  2. Anapigiwa kampeni huyo ili watuletee virus ndani ya club yetu.
    Hatutaki virus na vibaraka ndani ya club chama kubwa lenye malengo makubwa ndani na nje kisoka Simba sc

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic