JONAS Mkude, nyota wa Klabu ya Simba kwa sasa anasubiri simu ya Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez ili aweze kurejea kambini.
Kiungo huyo mkabaji kipenzi cha mashabiki na viongozi wa Simba alisimamishwa ndani ya Klabu hiyo Desemba 28 kutokana na utovu wa nidhamu.
Kwa mujibu wa Kamati ya Nidhamu ya Simba inayosimamiwa na Kamanda Mstaafu wa Kanda ya Dar, Seleman Kova iliweka wazi kuwa nyota huyo alikutwa na hatia ya makosa ya utovu wa nidhamu.
Kutokana na suala hilo alipigwa faini ya milioni moja na kupewa karipio kali pamoja na kutakiwa kuomba msamaha kwa njia ya maandishi ikiwa tayari ameshaomba msamaha kwa njia ya maneno.
Habari zinaeleza kuwa tayari ameshakamilisha kila kitu ikiwa ni pamoja na faini hivyo kwa sasa anasubiri ruhusu kutoka kwa CEO.
"Tayari Mkude amemaliza kila kitu kuanzia faini mpaka kuomba msamaha kwa maandishi, ni suala la simu ya CEO kwamba kijana rudi kazini anarudi kambini," ilieleza taarifa hiyo.
Chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes Mkude bado hajaanza mazoezi na hajashiriki pia Simba Super Cup ambapo leo timu yake itacheza na TP Mazembe kwenye mchezo wa kilele, Uwanja wa Mkapa.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa Mkude ni mali ya Simba na makosa aliyofanya ni sehemu ya kazi kwa binadamu.
Kitakacho mwondoa Mkude Simba: "wachezaji wenzake wamemgomea kuingia kambini hadi akose michezo 10."
ReplyDeleteUmesoma udaku umeamini..wenzio uzushi ndo mtaji wao kukunja hela
DeleteMkude amekiri makosa yake manaake anayekiri makosa yake hatoyarejea tena na yaliyomfika bila ya kuyata ni somo hatolisahau. Kutenda kosa ni sehemu ya maisha hara penseli mbele kuna risasi inayoandika na nyuma kuna kifutio cha kufuta makosa na. Mwenye nguvu ndie mwenye kusamehe, dhaifu ndie asiye samehe. Tunafahamu kabisa kuwa utovu wa Mkude umewaumiza sana wachezaji ambao Simba ndio maisha yao. Ombi ni tutumie uungwana wetu ili tumsamehe na hilo liwe funzo kwa wengine na huku Simba yetu Mungu azidi kuibariki na tunamfahamisha Mkude ajitulize kwani umri unampa kisogo na pia jina lako liwe linatajwa kuwa miongoni walioinogesha Simba kuliko kutajwa kwa ulikosa nidham na kufukuzwa
ReplyDeleteATARUDI KWENYE TIMU HILO HALINA SHIDA, SI UNAJUA KUNA AS VITA NA YANGA HAPO MBELE, THEN AL AHLY WANAKUJA?
Delete