HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa tayari wachezaji wa timu hiyo wamerudi kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili.
Mtibwa Sugar walivunja kambi baada ya kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na Simba visiwani Zanzibar.
Akizungumza na Saleh Jembe, Hitimana ambaye aliibuka ndani ya Mtibwa Sugar baada ya kufutwa kazi ndani ya Klabu ya Namungo FC amesema kuwa tayari maandalizi yameanza.
"Taratibu kwa sasa tumeanza maandalizi kwa ajili ya mechi zetu za Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili na nina amini kwamba tutakuwa imara.
"Ipo wazi kwamba mzunguko wa pili utakuwa na ushindani mkubwa ila mashabiki wasiwe na presha wazidi kutupa sapoti nina amini kwamba tutafanya vizuri na kila kitu kitakuwa sawa," .
Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 11 baada ya kucheza jumla ya mechi 18 na kibindoni ina pointi 22.
0 COMMENTS:
Post a Comment