January 20, 2021


 KOCHA Mkuu wa Azam FC, George Lwandamima amesema kuwa atawatumia nyota wake wapya leo kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Zanzibar Combine huku akikosa huduma ya ingizo jipya Yahya Zayd.

Zayd ambaye ni kiungo mshambuliaji yupo ndani ya Azam FC kwa mkopo wa miezi sita akitokea Klabu ya ENPPI ya Misri ambapo aliibukia huko msimu wa 2018 akitokea Klabu ya Azam FC.

Azam kwa sasa imeweka kambi visiwani Zanzibar ikiwa ni maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho ambapo kwenye Kombe la Mapinduzi waliishia kwenye hatua ya nusu fainali.

Ikiwa visiwani humo imecheza mechi mbili za kirafiki ya kwanza ilikuwa dhidi ya Mlandenge ambapo ilishinda mabao 2-0 na ule wa pili ilionja joto ya jiwe kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya KMKM.

Leo itakuwa Uwanja wa Amaan, kumenyana na Zanzibar Combine mchezo wa mwisho wa kufunga kambi Visiwani Zanzibar.

Lwandamina amesema:"Kila mchezaji yupo tayari na morali ni kubwa jambo ambalo linanipa furaha na kuona kwamba kila mchezaji anataka kuwa sehemu ya kikosi.

"Nitamkosa Zayd ambaye anaumwa Malaria huku kipa mpya Mathias (Kigonya) anaweza kuanza kucheza na wachezaji wengine wapo vizuri na wote wanapenda kuwa kwenye kikosi kitakachoanza dhidi ya Zanzibar, Combine," .



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic