January 20, 2021

 


PRESHA imezidi kuwa kubwa kwa Kocha Mkuu wa Chelsea, Frank Lampard ya kufutwa kazi kutokana na mwendo mbovu wa timu yake ndani ya Ligi Kuu England. 

Kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Leicester City,  Uwanja wa King Power kinawashusha kwa nafasi moja kutoka ile ya 7 mpaka ya 8 kikiwa na pointi zake 29 baada ya kucheza mechi 19.

Leicester City ambao walisepa na pointi tatu baada ya Wilfred Ndidi kupachika bao dakika ya 6 na James Maddison kupachika bao dakika ya 41  ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo na pointi zao ni 38 baada ya kucheza mechi 19.

Ikiwa  imecheza mechi tatu za Ligi Kuu England Januari imeshinda mchezo mmoja ilikuwa mbele ya Fulham ambapo ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Mason Mount dakika ya 78 baada ya Fulham kuwa pungufu kwa kuwa Antonee Robinson alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 44.

 Ilichapwa mabao 3-1 dhidi ya Manchester City na kichapo cha mabao 2-0  dhidi ya Leicester City ambao ni vinara wa Ligi Kuu England. 

Lampard amesema:"Ninadhani kwamba kwa sasa mambo bado hayajawa mazuri ila sio kazi rahisi kwa hapa ambapo nipo, ikiwa mabosi wataamua kwa namna nyingine sina mashaka,".

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic