January 20, 2021


 IMEELEZWA kuwa nyota wa Klabu ya Simba Jonas Mkude hukumu yake ipo palepale na kwa sasa anasubiri kupewa adhabu yake kutokana na makosa yake ya utovu wa nidhamu.

Kiungo huyo chaguo namba moja la makocha wote ambao wanapita ndani ya Simba kwa sasa yupo nje kidogo ya timu hiyo baada ya kusimamishwa mwishoni mwa mwaka 2020 kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu.

Habari zimeeleza kuwa licha ya Simba kugoma kuweka wazi makosa yake miongoni mwa sababu ambazo zilipelekea aweze kuwekwa kando ni pamoja na kuchelewa safari zote mbili za timu hiyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo ilikuwa ile ya kwenda Nigeria kwenye ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Plateau United.

Pia kwenye safari ya kwenda Zimbabwe ambapo ilipoteza Simba kwa kufungwa bao 1-0 na FC Platinum huku mtupiaji akiwa ni Perfect Chikwende ambaye kwa sasa ni mali ya Simba.

Mbali na hapo inaelezwa kuwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara wakati wanakwenda Mbeya kumalizana na Mbeya City, Mkude alichelewa jambo lililofanya viongozi wa Simba kongea naye ili aweze kubadili mwendo wake ila mambo yakawa ni yaleyale.

Chanzo kimeeleza kuwa kwa wakati huu adhabu yake ya kwanza ilikuwa ni kukosa mechi 10 baada ya wachezaji wa Simba kuomba iwe hivyo na tayari ameshakosa mechi saba za mashindano.

Mechi moja ilikuwa ni Kombe la Shirikisho moja ya ligi na mechi nne zilikuwa ni za Kombe la Mapinduzi huku moja ikiwa ni ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Mkude kwa sasa bado kesi yake inaendelea na hivi karibuni huku yake itatoka hivyo ni suala la kusubiri," .

Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema:"Suala la Mkude lipo kwenye kamati ya nidhamu muda ukifika wao watatoa majibu,".

9 COMMENTS:

  1. Hawa waandishi unprofessional sijui huwa wanaokotwa wapi. Mbaya zaidi kila mara wasomaji wamekuwa walikosoa makosa ya wazi ktk page hii lakini uongozi unapuuzia.

    Suala la Mkude wala hajawa Charged wala kuhukumiwa kwa kosa lolote. Mkude mpaka sasa hana hatia yoyote mpaka hapo atakaposikilizwa na kutolewa maamuzi. Suspension haina maana kuwa ni mhalifu, kusimamishwa kupisha uchunguzi.

    Hizo Mechi 10 aliadhibiwa na bibi yako????

    ReplyDelete
  2. Mchezaji hawi mchezaji mpendwa bila ya kuwa na nidham na nidham ndio inayojenga kiwango sio mpirani tu lakini kwa maendeleo yote katika maisha ya binaadamu na bila ya nidham hapana atayekukubali na kukuthamini

    ReplyDelete
  3. sasa wanamsimashaje wakat uchunguz unaendelea wakigundua hana atia itakuaje ? hap

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hata mtu akikaa mahabusu miaka minne na baadaye mahakamani akaja kuonekana hana hatia, huwa ndio imeisha hiyo, hakuna kulalamika

      Delete
  4. ukute huyu ndio kamkimbiza flaga duuu bongo noma bora wampige chini tu

    ReplyDelete
  5. Mkude anapendwa na mwenye timu , sisi tunajihangaisha tu .

    ReplyDelete
  6. Wanatumizngua tu ukwl wanaujua wao sisi tunataka ushindi tu .

    ReplyDelete
  7. Mapugufu yapo kwa kila binadam aliye hai hivyo kurekebishana ni kawaida

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic