JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa walistahili kushinda mchezo wa Ligi Kuu England usiku wa kuamkia leo mbele ya Tottenham inayonolewa na Kocha Mkuu, Jose Mourinho.
Ikiwa ugenini Uwanja wa Tottenham Hotspur iliweza kushinda mabao 3-1 na kusepa na pointi tatu ambapo ilianza kufunga bao la kwanza dakika ya 45+4 kupitia kwa Robert Firmino.
Spurs walipata bao kipindi cha pili kupitia kwa Pierre Emile Hojberg dakika ya 49 na kasi ya Liverpool iliendelea kupitia kwaTrent Alexander Arnold dakika ya 47 na msumari wa mwisho ulipachikwa na Sadio Mane dakika ya 65.
Klopp amesema:"Tulistahili kushinda na vijana walijituma nankutumia akili ndani ya uwanja kwani mchezo ulikuwa mgumu, ".
Mourinho amesema kuwa makosa ya ulinzi yamewaponza ndani ya dakika 90 jambo lililowafanya waweze kupoteza mchezo huo.
Ushindi huo unaifanya Liverpool kukusanya jumla ya pointi 37 ikiwa nafasi ya nne na Tottenham inabaki na pointi zake 33 ikiwa nafasi ya 6 na kinara ni Manchester City mwenye pointi 41.
0 COMMENTS:
Post a Comment