January 20, 2021

 


MTAMBO wa mabao ndani ya Klabu ya Namungo FC, Bigirimana Blaise atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu akitibu majeraha yake ya mguu.

Nyota huyo alipata majeraha hayo kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi Uwanja wa Amaan wakati timu yake ikikubali kichapo cha mabao 2-1 dhid ya Simba.

Alipata maumivu hayo dakika za lala salama wakati wa kugombea mpira na kipa namba mbili wa Simba, Beno Kakolanya.

Kwa mujibu wa daktari wa timu ya Namungo, Gabriel Kasonde amesema Blaise mwenye mabao manne ndani ya Ligi Kuu Bara atakaa nje kwa muda wa miezi mitatu.

"Atakaa nje ya uwanja wiki tatu kisha anaweza kukaa nje ya uwanja miezi mitatu wakati akirejea kwenye ubora wake taratibu na itategemea na namna hali yake itakavyokuwa, " .

Namungo ndani ya Ligi Kuu Bara imefunga jumla ya mabao 11 ipo nafasi ya 15 na pointi zake ni 18.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic