January 9, 2021


KOCHA Sven anatajwa kuibukia ndani ya Klabu ya F.A.R Rabat ya Morocco baada ya kubwaga manyanga ndani ya Klabu ya Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Kocha huyo amesaini dili la miaka miwili kuifundisha timu hiyo baada ya kupata dili nono lililomfanya asepe ndani ya Simba.



 Vandenbroeck alikuja Bongo msimu wa 2019/20 kupokea mikoba ya Patrick Aussems raia wa Ubelgiji ambaye alifutwa kazi na mabosi wa Simba kwa kile kilichoelezwa kuwa alishindwa kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa baada ya kutolewa na UD Songo hatua ya awali.


Kocha huyo alikiongoza kikosi cha Simba Januari 6 kufuzu hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kubwaga manyanga Januari 7 kwa kile alichoweka wazi kwamba ni masuala ya familia yalimuweka kando na timu hiyo.

Mbeligiji huyo ambaye Mtendaji Mkuu wa Simba, Babra Gonzale anatajwa kuzungumza naye kwa muda wa saa moja ili abaki amekwenda kuchukua nafasi ya kocha Abderrahim Talib ambaye amefukuzwa kazi.


8 COMMENTS:

  1. Kila lakheri Sven endelea kutengeneza CV binafsi kwangu ulikuwa kocha Bora umeondoka wakati timu as team ikiwa inakuitaji sana. Uwe na mafanikio mema

    ReplyDelete
  2. Waswahili wanasema ukisema wanini huyu? wenzako wanawza watampata lini. Watanzania tunatakiwa kuwa na adabu na kuheshimu taaluma za watu. Sven wenye kujua makocha tulijua mapema sana kuwa ni kocha hasa na alikuja Tanzania kufanya kazi.Na alikuwa yupo kiufundi zaidi yaani alihitaji muda ili kujenga msingi halisi wa kiuchezaji ndani ya simba ila maneno ya dharau na kejeli yalizidi mno.Nampongeza sana Mo na Barbara kwani nadhani ni miongoni mwa viongozi waliokuwa wametia pamba masikioni juu ya Sven na kumuacha kufanya kazi yake ila baadhi ya mashabiki wa simba ni wahovyo na wakiendekezwa wataipoteza timu wanapaswa kubadilika ikiwezekana wapewe elimu maalum ya mpira kwani wanajifanya wanajua wakati hawana wanachokijua. Kocha aliewahi kuwa msaidizi wa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Cameroon hadi kwenda kubeba kombe la mataifa ya Africa vipi unakwenda kumtilia shaka kufundisha timu kama simba? Sasa mwana kulitafuta mwana kulipata. Uwezekano wa simba kufanya vizuri kwenye ligi na klabu bingwa Africa itategemea bahati zaidi kwa maana yakwamba kocha atakaekuja aje kuanza na mafanikio lakini uwezekano wa simba kufanya vibaya ni mkubwa zaidi kama tutachukulia uhalisia wa kocha mgeni mpaka kuja kutengeneza mifumo yake ya kazi na kuzoea mazingira yote kwa ujumla.Na hapa ndipo wale waliokuwa wakimbeza sven watajua hawajui.Ni ushindi na furaha kwa Yanga kuelekea ubingwa.Yanga kama kuna kitu walikuwa wanakihofu kutoka simba katika mbio za bingwa si chengine bali ni mbinu za Sven.

    ReplyDelete
    Replies
    1. UMEANDIKA VIZURI LAKINI SIO FACT YA MSINGI SANA KUHUSU KUFANKIWA AU KUTOKUFANIKIWA KWA SIMBA! ITAKUWA FACT ENDAPO ATAKUJA KOCHA AMBAYE HAUJUI MPIRA WA AFRIKA, KOCHA KAAMUA KUONDOKA UTAMFANYA NINI? PIRE LECHANTRE AMEIKUTA SIMBA KATI KATI AKAFUNDISHA SIMBA WAKAWA MABINGWA. MAFANIKIO YA SIMBA NI JUU YA NANI ATAIFUNDISHA SIMBA NA ANAUJUA VIPI MPIRA WA AFRIKA BASI.....

      Delete
  3. Aende zake yeye sio bora kuliko simba

    ReplyDelete
  4. je mwandishi sio wewe uliyekurupuka juzi na kuandika kuwa huyo kocha kafukuzwa...Je kwa akili yako ya kisomi inawezekana kuwa juzi alifukuzwa na kuwa jana kapata kazi nyingine...msiwe mna kurupuka kuandika habari zenye vichwa vinavyokera..Basi andikeni na majina yenu tujue mjinga asiyejua ni nani...hii saleh jembe ndiyo sehemu pekee ambayo mtu anaandika andika tu upuuzi..ndiyo maana mnaogopa kuandika majina yenu..

    ReplyDelete
  5. Kweli Simba timu kubwa Sven kajiongeza kwenda timu kubwa wakati mwenzia Zahera wa mtaa wa pili akienda Gwambina hahaha ndo nimeelewa utofauti wa hivi vilabu

    ReplyDelete
  6. Kweli Simba timu kubwa Sven kajiongeza kwenda timu kubwa wakati mwwnzie Zahera wa mtaa wa pili akiishia Gwambina hahaha sasa ndo nimejua utofauti wa hizi timu mbili

    ReplyDelete
  7. Wakwapi wale mashabiki Waliokuwa wanamponda coach hachezeshi mastreka wawili? Leo kila mtu anamsifia coach kwavile ameondoka, kweli wa Bongo bendera fuata upepo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic