January 9, 2021


 KIKOSI cha Namungo FC leo Januari 9 kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jamhuri kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi uliochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.


Dakika 90 ambazozilikuwa na ushindani mkubwa Jamhuri ilikwama kuweka mzani sawa wala kupata bao la kufutia machozi mbele ya Namungo inayonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morroco.

Shukrani kwa Eric Kwizera ambaye alifunga bao dakika ya 41 ambalo lilidumu mpaka muda wa mapumziko kwenye mchezo huo.


Dakika ya 52 nyota wa Namungo FC naye alipeleka shukrani kwa mashabiki wake wa Zanzibar kwa kutupia bao na kuifanya jahazi la Namungo lizidi kufanya vizuri na lile la wapinzani likizama mazima.

Kwizera ambaye amechaguliwa kuwa mchezaji bora amesema:"Haikuwa kazi rahisi ushindani ulikuwa mkubwa ila kwa kuwa tumeshinda ni furaha kwetu," ,


Kwa sasa Namungo FC inasubiri matokeo ya mchezo kati ya Simba na Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa 8:15 ili kujua kama inaweza kupata nafasi ya kuwa 'best looser'.

Kwenye kundi A, Yanga imetinga hatua ya nusu fainali ikiwa na pointi nne huku Namungo ikiwa na pointi tatu na mabao mawili huku ile Jamhuri imetolewa jumla kwenye mashindano hayo ya Kombe la Jamhuri ikiwa na pointi moja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic