January 20, 2021

 


MOHAMED Hussein, mmachinga, Kocha Msaidizi wa Klabu ya Yanga Princess amesema kuwa anaamini kwamba wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba hawakupaswa kumsajili winga, Perfect Chikwende raia wa Zimbabwe kwa kuwa wanawachezaji wengi kwenye idara hiyo.

Simba ambayo kwa sasa ipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola imekamilisha usajili wa Chikwende kwa dili la miaka miwili huku ikielezwa kuwa dau lake ni milioni 127 la usajili wake.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mmachinga amesema kuwa kwa namna mahitaji ya kikosi cha Simba yalivyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Ligi Kuu Bara haikuwa na sababu ya kumvuta winga kwenye kikosi.

"Ninavyoona mimi kwa Simba kumsajili Chikwende ni maamuzi mazuri ila hayana faida hasa kwenye uhitaji na makosa ambayo yanaonekana ndani ya wawakilishi wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Inaonekana mbele ina safu kali ya ushambuliaji na kwa upande wa mawinga inao wengi wenye uwezo mkubwa ambao wanafunga na kutengeneza nafasi za kufunga hivyo itakuwa ngumu kwake kuweza kujenga ufalme mpya.

"Inahitaji kumpata beki mzuri wa kati ambaye atakuwa akituliza mashambulizi huku kwenye safu ya kiungo mkabaji pia ikiongeza nguvu ila kumleta winga kwa sasa naona bado ni maamuzi ambayo hayakupaswa kufanyika kwa sasa.

"Yote kwa yote ni mchezaji mzuri na usajili wao ni suala la kusubiri namna gani mambo yatakuwa kwenye mechi ambazo atacheza ila asifikirie kuwa mfalme kwa wakati huu," 

12 COMMENTS:

  1. Yaelekea usajili wa mabingwa wa Tanzania unawakera hadi makocha wa timu za wanawake. Kwani timu yake haijasajili mrundi mwingine? Mbona hamwongelei ili kubalance mzani? Yajayo yanafurahisha sana....

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama kuna hoja ya msingi aminifu ya kuhoji uasjili wa simba kwa chikwende basi lazima kwanza tuhoji wapi ulazima wa usajili wa Yanga kwa Dikson Job? Kuna lamin moro, bakari nondo,Abdallah shaibu,saidi juma makapu. Hapa pamekaaje? Chikwende ndie mchezaji pekee naona atakaekuja kuongezea simba nguvu halisi ya kutetea taji lake hakuna shaka na hilo

      Delete
  2. HUYU KOCHA NAE KIAZI KWELI! WE ULIAMBIWA SIMBA IMEMSAJILI CHIKWENDE KUJA KUJENGA UFALME? CHIKWENDE KALETWA AJE KUONGEZA NGUVU KATIKA SUALA LA KUWA MFALME NI JUHUDI ZAKE YEYE BINAFSI KUTAKA UFALME. FISTON KALETWA KUJENGA UFALME YANGA AU KUONGEZA NGUVU?

    ReplyDelete
  3. Simba haijakosea kumsajili winga Chikwende ambaye pia ni mfungaji na staili yake ya kumfuata beki akiwa na mpira ni faida kwa timu.Na isitoshe Simba inavyofanya ya kuongenza mawinga na washambuliaji ni wameangalia mbali kwa kufuatana na wachezaji walioko kwa sasa hasa kwa wachezaji kina Bocco, Mugalu, Kagere ni wahanga wa majeruhi yaani ni spana mkononi na sasa tunaelezwa pia BM huenda akafanyiwa operation.Yote kwa yote ukumbuke pia usajili wa wachezaji ni sawa na kamari tu kwa maana unaweza ukambulia galasa au uka hit jackpot kama ilivyo Simba na Konde boy.

    ReplyDelete
  4. Kila mtu ana Uhuru wa kutoa maoni yake lakini wakati mwingine Kuna maoni mengine unaona kabisa yamekaa kiushabiki tunaona hata timu kubwa duniani zinaweza zikawa na wachezaji hata watatu kwenye nafasi moja na bado wakasajili mtu mwingine kwenye nafasi hiyo hiyo mfano Man City,PSG

    ReplyDelete
  5. Ni mtazamo wake, wacha tuone uwezo wake uwanjani! Muda utaongea...

    ReplyDelete
  6. Ndio tuseme wanaitakia wema Simba au ni wivu tu?

    ReplyDelete
  7. Upo sahihi sana, kweli usajili kwa watani ila timu zetu hasa hizi kubwa zinakuwa na mihemko na usajili wa kuoneshana all in all tusubiri ujio wake km utaleta tija

    ReplyDelete
  8. usajili mzuri sana.big up viongozi wote simba sc.

    ReplyDelete
  9. nguruwe fc bila mchezaji kuwafunga hamuwezi kumsajili, mapaka fc nyie

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mliitwa Nyani tukajuwa jamaa katukana kumbe ni ukweli mtupu!

      Delete
    2. Ninyi hamkumsajili Nchimbi baada ya kuwapiga bao 3 saafi? Kwa ujumla Uto mmejawa na wivu. Nyie kwenye ulinzi mnae Lamine, Mwamnyeto, Ninja, Makapu n.k lakini mmemsajili beki mwingne Job wa nini?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic