January 20, 2021


 KOCHA Mkuu wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa amesema kuwa anaamini timu hiyo itafanya vizuri ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuwa ina wachezaji wazuri na wenye morali.

Ruvu Shooting kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 28 baada ya kucheza mechi 17.

Anashikilia rekodi ya kuwa mzawa wa kwanza ambaye amesepa na tuzo ya kocha bora ndani ya ligi ambayo ilikuwa ni ile ya mwezi Novemba.

Mkwasa amesema:"Ligi ina ushindani mkubwa hilo lipo wazi ila ninaamini kwamba uwepo wa wachezaji wazuri ndani ya timu yangu unanipa nguvu ya kuweza kufanya vizuri katika mechi zetu za ligi.

"Kikubwa ni kuona kwamba hapa kazi ni moja ya kupata matokeo na hilo linawezekana kwa kuwa kila mchezaji anahitaji ushindi na kupata matokeo mazuri," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic