INGIZO jipya ndani ya Klabu ya Simba ambaye ni winga Perfect Chikwende amesema kuwa anaamini atafanya vizuri ndani ya kikosi hicho ambacho kinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Chikwende amesaini dili la miaka miwili ambapo alitambulishwa rasmi Januari 16 kwa mashabiki wa Klabu ya Simba.
Aliibuka ndani ya Simba akitokea Klabu ya FC Platinum ambapo alionekana na Simba kupitia michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe, Chikwende alimtungua Aishi Manula wakati Simba ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0 ila kwenye mchezo wa pili uliochezwa Uwanja wa Mkapa Simba ilishinda mabao 4-0 na kutinga hatua ya Makundi Afrika.
Habari zinaeleza kuwa jina la nyota huyo limeachwa kwenye orodha ya wachezaji watakaoshiriki Ligi Kuu Bara huku nyota Francis Kahata yeye jina lake likiwa kwenye orodha ya wale watakoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Chikwende amesema:-"Ninafurahi kuwa ndani ya Simba, mashabiki wamekuwa nami kuona namna gani ninaweza kufanya vizuri kwenye kazi yangu ambayo ninafanya.
"Ukweli ni kwamba Simba ni timu kubwa nami nina amini kwamba nina kazi ya kufanya hivyo ni wakati wetu wa kuendelea kupeana sapoti ili kufnya vizuri,".
Karibu sana upige kazi ya kuonekana
ReplyDelete