HARUNA Niyonzima, kiungo mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa ndani ya uwanja amesema kuwa kwa kuwa wameanza na taji la Mapinduzi 2021, makombe mengine yanakuja zaidi.
Nyota huyo alikuwa ni nahodha visiwani Zanzibar na alikiongoza kikosi kwenye mechi zote nne ndani ya uwanja, ambapo kwenye dakika 360 walifungwa bao moja na kufunga mabao mawili.
Mabao hayo mawili waliifunga Namungo bao moja na sare ya kufungana bao 1-1 na Azam FC huku yeye akitengeneza pasi zote za mabao.
"Kazi kubwa ilikuwa ni kupambana kupata ubingwa wa Kombe la Mapinduzi, huu ni mwanzo ni muda wa kuendelea kuwa na furaha, mashabiki waendelee kutupa sapoti, makombe mengine yanakuja".
Sawa, ndio lengo la kila timu makini
ReplyDeleteYaani mechi nne wamefunga mabao mawili tu!
ReplyDeleteLabda kuwe Kuna penalti penalti na timu nyingine zichezeshe vikosi vya pili ndio makombe mengine yatakuja
ReplyDeleteLabda msubiri mapinduzi tena msimu ujao
ReplyDeleteNyie huko kwenye mapinduzi hamkuwepo au ndio akiri za kimanara hizo
ReplyDeleteLigi yenyewe mumechezea za wanaume wa wili bado mnajita kikosi kipana sijui mumepanuka wapi maana upana wenu hatuoni mpaka mwenye timu yake chama awepo ndio mshide kk kweli nyie
ReplyDeleteLigi haijaisha wewe utopolo
Delete