KOCHA Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solkjaer amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya kupata pointi tatu muhimu kwenye mchezo wa leo wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool.
Manchester United ambayo imekuwa na matokeo mazuri kwenye mechi zake za hivi karibuni ndani ya Ligi Kuu England inakutana leo na Liverpool ambao ni mabingwa watetezi kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja wa Anfield.
Ikiwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 17 kibindoni ina pointi 36 inakutana na Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wakiwa nafasi ya pili na pointi 33.
Ole amesema:"Hatuna ugeni na mchezo wetu dhidi ya Liverpool ambapo tutakuwa ndani ya Anfield ni jambo la kawaida kuwa nje na nyumbani pia ila tunahitaji ushindi ndani ya uwanja.
"Utakuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa ila tunahitaji pointi tatu ili kupata matokeo mazuri kikubwa ni suala la kusubiri na kuona itakuaje, tupo tayari," .
Jurgen Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa mchezo wa leo kwa kuwa wamejipanga vizuri.
Mchezo huo unatarajiwa kuanza kupigwa majira ya saa 1:30 usiku.
0 COMMENTS:
Post a Comment